Rasmi uongozi wa Yanga umemalizana na beki wake wa kati Andrew Vicent ‘Dante’ na kujiunga na kambi ya timu hiyo huku akiahidi kuendelea kuipambania timu hiyo kama ilivyokuwa awali.

Beki huyo anarejea na kujiunga na Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri wa timu hiyo baada ya miezi kadhaa kukaa nje ya timu hiyo akishinikiza kulipwa stahiki zake fedha za usajili alizokuwa akidai ambazo ni Sh Mil. 50.

Awali, uongozi wa Yanga ulikubali kumlipa fedha hizo kwa mafungu kabla ya kukataa na kwenda kushtaki TFF ambayo wiki iliyopita ilitoa hukumu kwa kumtaka beki huyo arejee kwenye kituo cha kazi huku akiendelea kulipwa madai hayo.

Dante alisema kuwa tayari wamefikia makubaliano mazuri na viongozi wa Yanga, jana aliripoti kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo na kufanya kikao na mwenyekiti wa timu hiyo, David Ruhago.

Dante alisema kuwa anashukuru wamemalizana vizuri na viongozi huku akiahidi kurejea kuipigania timu hiyo na kikubwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara unaotetewa na Simba.

“Nashukuru nimerejea nyumbani, nimekuja kufanya kazi na nitazidi kufanyakazi kama ilivyokuwa awali nikiipambania timu yangu kwenye misimu iliyopita.

“Nisingependa kuzungumza mengi hivi sasa, zaidi mtaniona nikiwa uwanjani nikiipambania timu yangu yenye malengo ya kuuchukua ubingwa wa ligi,” alisema Dante.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.