Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba jana wameendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na Kombe la Shirikisho la Soka nchini maarufu FA Cup dhidi ya Arusha United pamoja na michezo ya Ligi Kuu.

Kutokana na mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Bara yaliyofanywa na Bodi ya Ligi hivi karibuni, Simba itacheza mechi tatu Uwanja wa Uhuru kabla ya Januari 4, mwakani kuvaana na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuikaribisha Arusha United kwenye mechi ya Kombe la FA, Desemba 25 itavaana na Lipuli FC huku siku tatu baadaye ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya KMC FC kabla ya kufunga mwaka kwa kuikaribisha Ndanda FC hapo Desemba 31, mwaka huu.

Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola alisema wachezaji wa kikosi hicho wapo vizuri wakati huu wakiendelea na mazoezi na kufafanua kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

"Tunaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano ya Ligi Kuu," alisema Matola ambaye ataanza kukiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza msimu huu akiwa na Kocha Mkuu Mbelgiji Sven Vandenbroeck baada ya
Patrick Aussems kutimuliwa.

Naye msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara akizungumzia usajili wa dirisha dogo, alisema kwa upande wao hawana pupa na kudai watasajili kwa matakwa ya kocha wao ambaye anaendelea kukisoma kikosi hicho baada ya kukikabidhiwa hivi karibuni.

Alisema endapo kocha atahitaji kuongeza au kupunguza mchezaji yeyote, watasajili na kudai wapo imara idara zote kwa sasa.

"Sisi hatuna pupa ya usajili tutasajili kwa matakwa ya kocha wetu hatusajili kwa ajili ya kufurahisha watu," alisema Manara.

Aliendelea kusema wanaendelea kujipanga kwa ajili ya kukutana na mahasimu wao Yanga, Januari 4 Mwakani.

"Yanga wasajili kila siku, lakini tukutane Januari 4 Taifa," alisema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.