KUTOKANA na changamoto ya Uwanja wa kutumika kwenye mchezo wa kesho kati ya Tanzania Prisons na Yanga kuna hatihati ya mchezo huo kupangiwa siku nyingine.
Uwanja wa Sokoine ambao Mbeya City na Tanzania Prison zinazoshiriki Ligi Kuu Bara huutumia umezuiwa kwa muda na Bodi ya Ligi Tanzania kutokana na kutokuwa bora kwa saa baada ya usiku wa kuamkia leo kufanyika shughuli nyingine ya kijamii ambayo imeondoa ubora wa sehemu ya kuchezea.
Habari zinaeleza kuwa uongozi wa Tanzania Prisons na Yanga umekaa chini na kujadii eneo jingine la kuchezea na kupata changamoto ileile jambo ambalo linaashiria kuwa mechi hiyo inayweza kupangiwa tarehe nyingine.
Timu zote mbili leo zimeshindwa kufanya mazoezi kwenye uwanja huo kwa aiili ya kujiaandaa na mechi hiyo
Post a Comment