Kaimu mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda amesema kuwa ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Yanga Januari 4, basi wachezaji wanatakiwa wasiidharau timu hiyo ambayo inatumia dirisha dogo kujipanga upya.
Simba na Yanga zinacheza kwa mara ya kwanza katika mzunguko wa kwanza wa ligi msimu huu, Januari 4, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kaduguda alisema kuwa: “Wachezaji wanatakiwa waiheshimu Yanga pamoja na kuiona haipo sawa kwa sasa.
"Lakini watambue kuwa Yanga pindi inapocheza na Simba hubadilika kabisa wanakuwa timu nyingine na hawatacheza kama wanavyochezaga na Mtibwa au Mwadui, hivyo wanatakiwa waiheshimu Yanga.
"Lakini kubwa zaidi kwa upande wetu kama Simba ni kuhakikisha tunapata ushindi dhidi yao."
Post a Comment