KOCHA Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa kichapo cha mabao 2-0 walichokipata mbele ya Chelsea haimaanishi kuwa wapinzani wao ni bora bali waliwazidi maarifa kipindi cha kwanza huku akilaani vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Mourinho akiwa kwenye benchi la ufundi alishuhudia mabao hayo dakika ya 12 na 45 lililopachikwa kwa mkwaju wa penalti na da Silva Willian ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kufunga mabao yote mawili ya ushindi.
"Haina maana kwamba wao ni bora kisa wametufunga mabao hayo hapana ila walituzidi ujanja kipindi cha kwanza wakatumia nafasi ambazo wamezitengeneza zikawapa ushindi.
"Walikuwa bora kwa mchezaji mmojammoja kuanzia Kante, Wilian jambo ambalo lilionyesha kwamba walijipanga vema kupata ushindi kwangu, wanastahili pogezi,"
"Nimeskia kwamba kumekuwa na tatizo la ubaguzi wa rangi, nimeongea na nahodha wao Azplicueta kwa undani ili kujua kwamba ni kwa namna gani limetokea, sipendi kuona hili suala linaendelea na ni baya sana kwenye dunia ya sasa," amesema.
Tottenham ilimaliza mpira ikiwa pungufu baada ya kiungo wao Son Heung-min kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 62 kwa kumchezea rafu Antonio Rudiger
Post a Comment