Aliyekuwa straika wa Yanga, Juma Balinya, amesema ameondoka Tanzania na akiamini ipo siku atarejea tena. Imeelezwa.
Balinya ambaye alisajiliwa kabla ya msimu huu kuanza, ameichezea Yanga takribani mechi saba pekee kabla ya kuvunja mkataba wake.
Balinya ameeleza kuwa anaondoka Tanzania lakini ipo siku atarejea sababu maisha ya mpira ni popote.
"Huu ni mpira, naondoka lakini naamini ipo siku nitarejea," alisema.
Mashabiki Simba wanasemaje
Baada ya kuondoka kwa Balinya pale Yanga, baadhi ya mashabiki Simba wamesema endapo mchezaji huyo atatua kwao kuna uwezekano akang'ara zaidi.
Baadhi yao wameeleza kuwa Yanga hakupewa na nafasi na kutokana na kung'ara Uganda kabla hajatua Jangwani wanaamini anaweza akafunga zaidi akipata nafasi ya kucheza na Meddie Kagere
Post a Comment