MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool leo wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya kikosi cha Red Bull.

Kipindi cha kwanza mambo yalionekana kuwa magumu kwa Liverpool kutokana na kwenda mapumziko bila kufungana jambo lililomfanya Jurgen Kllopp Kocha Mkuu wa Liverpool kutumia muda huo kuwajaza maneno wachezaji wake.

Kipindi cha pili Liverpool iliandaka bao la kwanza dakika ya 57 kupitia kwa Naby Keita kabla ya dakika moja mbele Mohamed Salah kufunga bao la pili dakika ya 58.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kutinga hatua ya 16 Bora kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.