Baada ya Azam kusema kuwa imemalizana na klabu ya Yanga kuhusu Mshambuliaji Ditram Nchimbi, usajili wa mshambuliaji huyo umechukua sura mpya baada ya klabu yake anayoichezea kwa mkopo ya Polisi Tanzania kusema kuwa bado inamtambua Nchimbi kama mchezaji wao mpaka msimu wa 2019/2020 utakapomalizika.

Kaimu Katibu Mkuu na Afisa habari wa Klabu hiyo Frank Lukwaro akizingumza na gazeti hili amesema Azam waliwapa mchezaji huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja hivyo suala la wao kumalizana na Yanga ni hatua moja hivyo Yanga wanapaswa kuja mezani kwa ajili ya kumalizana na Polisi Tanzania kwakuwa bado ni mtumishi wao kwa mujibu wa taratibu za usajili wa mchezaji kwa njia ya mkopo (Loan Transfers) zilizomleta kucheza ndani ya Vijana hao ambao makazi yao ni Shule ya Polisi Tanzania zamani Ikijulikana kama CCP mkoani Kilimanjaro.

"Huyu ni mchezaji wetu kwa sasa pamoja na kwamba alikuwa mali ya azam lakini sisi ndio mabosi wake kwa sasa na hata Azam wiki iliyopota walimuomba arudi kwao kabla ya msimu tukakataa kwakuwa hayakuwa makubaliano yetu ya awali yaliyomleta kwetu ambayo yanasema atacheza kwa msimu mzima na sasa msimu bado haujaisha.

"Kilichopo ni dirisha dogo ambapo kama wanahitaji huduma yake na sisi tunapaswa kushirikishwa kwa sababu tulishamuweka katika mipango yetu " Alisema Lukwaro.

Alisema baada ya kusikia azam wamemtangaza Nchimbi kuwa ni mali ya Yanga kwa sasa wanawasubiri Yanga mezani ili waweze kumalizana nao na hakuna ujanja kwakuwa wao ndio wenye uhalali.

Aidha, Lukwaro alisema wao hawawezi kumbania mchezaji yeyote kwenda klabu anayoitaka ispokuwa wanachohitaji ni taratibu kufuatwa ambapo aliongeza kuwa katika wamewekeza mambo mengi mpaka Nchimbi kurudia makali yake hivyo ni lazima Azam na Yanga wawaheshimu

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.