Liverpool, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu sita zinazotaka kumsaini mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na Paris St-Germain Neymar, 27, na mchezaji mwenzake Kylian Mbappe, 20. (Le Parisien, via Mirror)
Mbappe ambaye ni mshambuliaji wa Ufaransa hana mpango wa kusaini kandarasi mpya PSG mkataba wake wa sasa ukimalizika mwisho wa mwaka 2022. (Marca)
Carlo Ancelotti ndiye chaguo la Everton atakayemrithi Marco Silva kama mkufunzi baada ya Mtaliano huyo kufutwa kazi na Napoli usiku wa Jumanne. (Telegraph)
Manchester City inamhitaji beki mpya na tayari imejiunga na foleni ya usajili wa nyota wa Ufaransa Samuel Umtiti, 26, kutoka Barcelona. (L'Equipe, via TEAMtalk)
Wakimkosa Umtiti, Manchester City itaelekea Bournemouth kumtafuta Nathan Ake, 24, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea. (Express)
Beki wa England Fikayo Tomori, 21, anakaribia kusaini mkataba mpya Chelsea. (Goal)
Zlatan Ibrahimovic huenda akarejea tena katika ligi ya Premia baada ya Everton kumpatia ajenti wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi wa miaka 38-ofa ya £4m. (Express)
Manchester United huenda ikamkosa kiungo wa kati wa England James Maddison, 23, ambaye anakaribia kutia saini mkataba mpya ulioimarishwa Leicester City. (Mirror)
Roman Abramovich amepuuzilia mbali ofa kutoka kwa mmiliki wa LA Dodgers, odd Boehly kununua klabu ya Chelsea. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez amesema anafurahia sana kucheza katika vilabu vikubwa lakini siku zijazo angelipendelea kurejea katika ligi kuu ya Uhispania, La Liga. (Mail)
Mkufunzi wa Inter Antonio Conte anataka Chelsea imuachilie beki wa nyuma na kushoto Mhispania Marcos Alonso, 28, ili aungane nae Italia huku winga Pedro, 32, na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, pia wakitarajiwa kuondoka Stamford Bridge. (Goal.com)
Barcelona wamesitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22 kutokana na bei ya 100m euro (£84.6m. (ESPN)
Liverpool na Manchester City wamewasilisha ofa ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Inter Sebastiano Esposito,17. (FCInterNews, via Sporting Witness)
Marudio ya mchuano wa El Clasico kati ya Barcelona na Real Madrid huenda ukaahirishwa tena baada ya kubainika kuwa waandamanaji 18,000 wanapanga kuzua rubsha. (Mail)
Post a Comment