Baada ya watani zao wa jadi Yanga kuanza usajili kwa kasi, uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kamwe hautoweza kufanua usajili wa fasheni.
Manara ameeleza kuwa usajili ambao wanaufanya Yanga hauwezi kuwayumbisha nao wafanye usajili sababu ya mihemko ambayo haina maana.
Ameeleza kuwa Simba inasikiliza mapendekezo ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na si kutazama kipi watani zao wa jadi wanafanya.
"Sisi hatuwezi kufanya usajili sababu ya wenzetu.
"Simba ni taasisi ambayo inafanya kazi kiueledi hivyo tunasubiri mapendekezo ya kocha wetu ndipo litafanyika hilo."
Kwa upande mwingine, Manara amesema wala hawatishwi na usajili ambao Yanga wanaufanya hivi sasa akiamini hauwezi kuwa na tishio kwao
Post a Comment