Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo imeshida mchezo wake wa kwanza mbele ya Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Mchezo wa kwanza wa ufunguzi Kilimanjaro Stars ilipoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Kenya lililopachikwa dakika ya nne.
Bao pekee la Kilimanjaro limepachikwa dakika ya 38 baada ya mlinda mlango wa Zanzibar Heroes kuutema mpira uliopigwa na Eliuter Mpepo ukakutana na Ditram Nchimbi ndani ya 18.
Michuano hiyo inafanyika nchini Uganda ambapo kwenye mchezo mwingine Kenya ilishinda bao 1-0 dhidi ya Sudan.
Post a Comment