Kaimu mwenyekiti wa Simba,Mwina Kaduguda amewataka wanachama wa Simba kuhakikisha wanazitumia vyema kadi za kisasa ili kuongeza kipato cha klabu hiyo.
Amesema Simba ina kiu ya kuchukua mataji ya ubingwa wa Ligi Kuu bara na hata ubingwa wa Afrika, hivyo zinahitajika pesa za kutosha kuendesha klabu hiyo.
"Tunahitaji kuiangusha TP Mazembe na hatuwezi kufanikiwa kwa maneno maneno, vinatakiwa vitendo ndio maana tumebuni kadi za kisasa ambazo zitakuwa zinatuingizia pesa.Lazima tubadilike kuhakikisha tunafanya mambo kisasa ili tufanye makubwa Afrika.
"Tukawe mabalozi kwa wengine ambao hawajafika hapa maana pamoja na klabu kunufaika pia mnaweza kukopeshwa bodaboda na bajaji," amesema Kaduguda.
Idadi ya wanachama waliojitokeza katika uzinduzi huo ilikuwa ndogo huku sababu ikitajwa kwamba hawakutangazwa ipasavyo kwa kuhofia vurugu.
Post a Comment