Uongozi wa klabu ya Yanga umezidi kuwasisitiza wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi juu ya usajili wa dirisha dogo.
Dirisha dogo la usajili kwa klabu za Ligi Kuu nchini limefunguliwa rasmi jana na sasa timu zote husika zinaruhusiwa kusajili kulingana na mapungufu waliyonayo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ameeleza kuwa watafanya usajili huo vizuri kulingana na mahitaji ya kocha.
Aidha, kwa upande mwingine Bumbuli ameeleza kuelekea mechi yao na Simba wamejipanga vilivyo.
Ameeleza maendeleo yanaenda vema na akisema hawawezi kuanika mikakati yao hadharani lakini watakionesha cha moto kwa mnyama.
Yanga na Simba zinatarajia kukutana Januari 4 mwakani katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Post a Comment