MIKEL Arteta, Kocha Mkuu mpya wa Arsenal amesema kuwa atatumia nguvu kubwa kuwashawishi wachezaji wake watumie uwezo wote walionao kupata matokeo.

Arteta amechukua mikoba ya Unai Emery ambaye alipigwa chini hivi karibuni baada ya kudumu kwa muda wa miezi 18 amepewa kandarasi ya miaka mitatu na nusu kukinoa kikosi hicho.

Arteta ambaye aliwahi kucheza ndani ya Arsenal na alikuwa nahodha amesema kuwa anaamini wachezaji wanaweza kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mashabiki na timu kiujumla.

"Nitawashawishi wachezaji kucheza kwa nguvu na kutumia uwezo wao wote walionao kupata matokeo chanya.

"Hatua kwa hatua ninaamini kwamba tutafikia malengo yetu na mafanikio tutayaona yatakayotutambulisha sisi katika wakati ambao tunauhitaji," amesema.

Kabla ya kutua Arsenal, Arteta alikuwa ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi Manchester City akifanya kazi na Kocha Mkuu, Pep Guardiola

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.