Ni kama Yanga wameanza kuleta silaha tayari kwa ajili ya kuelekea mechi yao na Simba baada ya kumshusha straika Tariq Seif aliyekuwa akipiga soka Misri.

Sefi ambaye awali aliwahi kuzichezea timu za Biashara United na Stand United za hapa Tanzania, aliondoka kuelekea Misri ambapo alikuwa akiichezea Dekeners FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

Seif na Yanga wameshamalizana kila kitu na panapo majaliwa leo ama kesho anaweza akaondoka kuelekea Kigoma ambapo Yanga itaweka kambi ya muda mfupi.

Straika huyo anatajwa kuwa mbadala wa Juma Balinya ambaye amevunja mkataba na Yanga ambayo imetangaza rasmi juzi kuwa wamekubaliana kuachana

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.