SVEN Vanderbroek Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji na Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi wana kibarua kizito ndani ya dakika 270 ambazo ni sawa na mechi tatu kusaka pointi tisa za kufungia mwaka 2019.
Simba ambayo iliongozwa na Patrick Aussems aliyefukuzwa baada ya kuongoza mechi 10 za ligi, ilishinda mechi 8 na kuambulia sare moja mbele ya Tanzania Prisons na kupoteza mechi moja mbele ya Mwadui FC ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 25 itaanza kuzimega dakika 270 za hatari Jumatano ya leo Desemba 25.
Vanderbroek tayari ameonja utamu wa benchi la Simba kwa kupata ushindi wa mabao 6-0 mchezo wake wa kwanza ambao ulikuwa ni wa kombe la Shirikisho mbele ya Arusha FC leo atakaa benchi kwenye mchezo wa kwanza utakaochezwa uwanja wa Uhuru.
Simba itamenyana na Lipuli ya Iringa Desemba 25 kisha Desemba 28 itamenyana na KMC kabla ya kufunga mwaka na Ndanda FC Desemba 31 kukamilisha dakika 270 za hatari za kusaka pointi tatu zitakazochezwa uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Seleman Matola amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mechi zao zote na zinaugumu wa kutosha jambo ambalo linawafanya wazipigie hesabu kwa umakini na kuwataka mashabiki wajitokeze
Post a Comment