Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Simba, Mohammed Banka, amewashauri mabosi wa klabu hiyo kumpa uhuru kocha mpya Sven Vandenbroeck, muda wa kujenga kikosi.
Banka ameamua kufunguka hayo kutokana na tamaduni ya timu za hapa nyumbani kutotoa nafasi kwa makocha ambao wamekuwa wakifanya vibaya kwa muda mfupi.
Kiungo huyo aliyekuwa mjanja-mjanja wakati akiichezea Simba, ameeleza ni nafasi ya kumpa muda kocha huyo aoneshe kile alichonacho kutokana na uzoefu wake.
Ameeleza kwa kusema kuwa kama atafeli ndani ya msimu isiwe sababu ya Simba kufanya maamuzi dhidi yake bali wamuache aendelee kukijenga zaidi kikosi cha timu hiyo.
Post a Comment