Wakati ikidizi kujiimarisha katika usajili wa dirisha dogo kwa kusajili wachezaji nyota wa kuziba mapengo yaliyojitokeza, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, ametajwa kuwa ni miongoni mwa makocha walioomba kazi ya kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria nchini,
Klabu ya Yanga, imeele

Tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo Desema 16, mwaka huu, Yanga inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa baada ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera kutimuliwa, imekuwa 'bize' na usajili huku suala la kutafuta kocha mkuu likionekana kupoa kwa sasa.

Hata hivyo, juzi usiku ziliibuka taarifa kuwa Aussems ni miongoni mwa makocha walioomba kuinoa timu hiyo iliyopo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 17 baada ya kushuka dimbani mara nane msimu huu.

Lakini alipoulizwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo zaidi ya kusema kwa sasa wanashughulikia kwanza usajili na hana taarifa hizo za Aussems kuomba kazi katika klabu hiyo.

"Sina taarifa hizo, kama kuna kitu kama hicho hakijafika mezani kwangu, naomba muwe na subra kwanza kwa sasa," alisema.

Kwa upande wa usajili, klabu hiyo imefanikiwa rasmi kuinasa saini ya kiungo mnyumbulifu, Mnyarwanda Haruna Niyonzima anayeitumikia AS Kigali ya kwao, Rwanda sambamba na straika Ditram Nchimbi aliyekuwa akiichezea Polisi Tanzania kwa mkopo akitokea Azam FC.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mhandsi Hersi Said, ndiye aliyemtambulisha Niyonzima baada ya kusaini mkataba wa kujiunga tena na timu hiyo mjini Kigali jana hiyo ikiwa ni baada ya juzi kumtambulisha Nchimbi kufuatia kutia saini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na miamba hiyo akiwa jijini Kampala, Uganda kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika
Alhamisi wiki hii.

Wakati usajili ukikamilika kwa wachezaji hao ambao sasa wanaungana na Tariq Seif, na beki wa kushoto Adeyun Saleh Ahmad waliosajiliwa katika dirisha hili, Mkurugenzi wa Mashindano wa klabu hiyo, Thabit Kandoro jana alimpokea mshambuliaji Muivory Coast, Gislein Yikpe Gnamian aliyekuwa anachezea Gor Mahia ya Kenya baada ya kuwasili kwa ajili ya kujiunga na Yanga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.