LAMINE Moro, beki wa Yanga ambaye aliondoka hivi karibuni kutokana na madai ya mshahara na kurejea nchini Ghana inaelezwa kuwa amerejea Bongo kumalizana na mabosi wake hao.
Moro alikuwa bora kwenye mechi zake ambazo alizicheza akiwa na Yanga msimu huu.
Habari zinaeleza kuwa tayari amemalizana na Yanga ambao wanatarajia kucheza na Simba Januari 4 mwakani.
Moro alihusishwa kutua ndani ya Simba ambao walifanya naye majaribio na kuamua kumuacha na ilielezwa kuwa alikuwa anahitajika kwa sasa ili akaitumikie klabu hiyo yenye maskani yake Kariakoo.
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alisema kuwa Moro bado ni mchezaji wa Yanga kwa kuwa bado anamkataba ndani ya timu hiyo.
Post a Comment