Imeripotiwa kuwa mabosi wa Yanga wameanza kufanya mawasiliano na winga wa kimataifa wa Msumbiji na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Luis José Muquussone.

Yanga wameanza mazungumzo na straika huyo anayecheza kwa mkopo UD Songo ya Msumbiji ili kumsajili katika dirisha dogo la usajili ambalo linafunguliwa Jumatatu ya wiki ijayo.

Muquussone anakumbukwa kwa kuifunga Simba katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1.

Usajili huu wanaupigania Yanga wakiwa wametoka kumalizana na Tariq Seif ambaye alikuwa akikipa huko Misri katika Ligi Daraja la Pili.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.