FREDDIE Ljungberg, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Arsenal amepata ushindi wake wa kwanza akiwa kwenye benchi la Arsenal kwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya West Ham mchezo wa Ligi Kuu England.

Arsenal ilimpiga chini Unai Emery ambaye alidumu Kwa muda wa miezi 18 kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi Jambo lililowafanya mabosi waamue kuachana na Unai jumla.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Gabriel Martinell dakika ya 60, Nicolas Pepe dakika ya 66 na msumari wa mwisho ulipigwa na Pierre Aubameyang dakika 69 na lile la West Ham likipachikwa na Angelo Ogbonna dakika ya 28.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya pointi 22 ikiwa nafasi ya tisa huku West Ham ikiwa nafasi ya 16 na ina pointi 16 zote zimecheza mechi 16 kinara ni Liverpool mwenye pointi 46.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.