KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, ameweka wazi kuwa amepanga kumsajili mshambuliaji raia wa Ubelgiji, Andréa Fileccia mwenye umri wa miaka 28.
Nyota huyo anakipiga katika Klabu ya Royal Francs Borains ya nchini Ubelgiji katika kipindi anaweza kutua kipindi cha usajili wa dirisha kubwa kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Kwa sasa Eymael yuko nchini Ubelgiji ambapo alirejea baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona na anaweza kurejea muda wowote anga likifunguliwa kwani ligi inatarajiwa kuanza Juni Mosi.
Eymael amesema kuwa, amepanga kumsajili mshambuliaji huyo ambaye atakuja kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Yanga na tayari aliwaachia viongozi wa Yanga jina la mchezaji kwa ajili ya kukamilisha dili hilo mapema kabla ya kuingia kambini kujiandaa na ligi ya msimu ujao.
Eymael aliongeza kuwa, dili hilo huenda likakamilika kirahisi kwa sababu amewahi kumfundisha mchezaji huyo wakati yupo Afrika Kusini
Post a Comment