WACHEZAJI wa Simba leo baada ya kuwasili kambini wamefanyiwa vipimo vya afya ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kuelekea maandalizi ya kumaliza mechi za mzunguko wa pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa wapo kambini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

'Tumeshawasili kambini na wachezaji wameanza kuripoti, kikubwa ambacho kinafanyika ni kuanza kuwafanyia vipimo ili kujua afya zao kisha program nyingine zitafuata,"

Miongoni mwa wachezaji ambao wamewasili kambini leo ni pamoja na nahodha msaidizi Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Beno Kakolanya na Said Ndemla.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.