UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mastaa wote wa timu hiyo waliopo Tanzania wataingia kambini mapema kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja kuanza kuelekea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vmbi Juni Mosi.

Ligi Kuu Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Viriusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia na inatarajiwa kurejea hivi karibuni baada ya Serikali kusema kuwa hali ya maambukizi imeanza kupungua.

Akizungumza na Seleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana imani wachezaji wote wataingia kambini kwa wakati.

"Wachezaji wengi wote wapo nchini isipokuwa mmoja tu Farouk Shkalo yeye yupo Kenya utaratibu unafanyika ili aweze kurejea.

"Kwa upande wa benchi la ufundi ni mpaka pale mambo yatakapokuwa shwari kwani huko kwao mipaka bado haijafunguliwa itakapofunguliwa tu watarejea kuungana na timu," amesema.

Leo mastaa wa klabu hiyo baadhi wameanza kuripoti ambapo wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.