UONGOZI wa Simba umesema kuwa bado unaendelea kufanya mawasiliano na nyota wao ambao hawajawasili kambini ili kujua namna gani wataweza kuja Bongo.

Miongoni mwa wachezaji wa kigeni waliokwama kutua Bongo ni Francis Kahata aliyepo Kenya, Sharaf Shiboub aliyepo Sudan na Clatous Chama ambaye yupo Zambia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa nyota hao bado hawajatua nchini utaratibu unaendelea ili kuona namna gani wataungana na wengine.

"Tunategemea hivi karibuni mambo yakiwa sawa wanaweza kuungana na wenzao ila kwa sasa mambo bado kutokana na mipaka yao kufungwa hivyo tunaangalia namna itakayowezekana kuwarejesha.

"Tayari wachezaji waliopo ndani wameanza kuripoti kambini na baada ya kumaliza kufanyiwa vipimo wanaweza kuanza mazoezi ila itategemea na muda tutakaomaliza vipimo," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.