JOSHUA Kimmich raia wa Ujerumani, kiraka anayekipiga ndani ya Klabu ya Bayern Munich alizima ndoto za Dortmund kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa Bundesliga uliopigwa jana.
Bao pekee la kiraka huyo lilijazwa kimiani dakika ya 43 kipindi cha kwanza na kuwafanya wapinzani wao washindwe kufurukuta mbele ya Bayern Munich waliosepa na pointi tatu mazima.
Ushindi wa jana unaifanya Dortmund ishindwe kufuta uteja mbele ya Bayern Munich ambao kwenye Ligi tangu msimu wa 2012/13 wakiwa wamekutana mara 16,Munich wamepoteza mara tatu na sare tatu huku mechi 10 Munich wakisepa na ushindi.
Matokeo hayo yanaifanya Bayern Munich kujikita nafasi ya kwanza na pointi zake 64 huku Dortmund ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 57 zote zimecheza mechi 28.
Nyota wa Dortmund, Erling Haaland alipata majeraha kipindi cha pili kwenye gemu hiyo iliyokuwa na ushindani licha ya kutokuwa na mashabiki.
Post a Comment