KIUNGO Mzambia anayekipiga kunako kikosi cha Simba, Clatous Chama, amesema akiwa anacheza kwa kushambulia akitokea upande wa kushoto, anakuwa mtamu zaidi kuliko nafasi nyingine uwanjani.
Msimu uliopita ulikuwa bora zaidi kwa Chama kwani alifanya mambo makubwa akifunga na kutoa pasi za mabao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuisaidia Simba kufi ka robo fainali.
“Licha ya kwamba mimi ni mchezaji ninayeamini kwenye kucheza kitimu, hivyo na-kuwa tayari kucheza katika na-fasi yoyote uwanjani ili kuisaidia timu yangu.
“Lakini nimekuwa huru na ku-fanya vizuri zaidi endapo kocha akinipa majukumu ya kucheza nafasi ya winga hasa ile inayoniruhu-su kusham-bulia nikitokea upande wa kushoto,” alisema Chama.
Post a Comment