HASSAN Dilunga, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba ni miongoni mwa nyota ambao tayari wameanza mazoezi ya pamoja na timu yake.
Mei 27 Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara waliripoti kambini na kufanyiwa vipimo vya afya kisha jioni walianza kufanya mazoezi mepesi ikiwa ni maandalizi ya awali kabla ya kurejea kwenye mechi za ushindani.
Hakukuwa na mechi ya ushindani ndani ya Bongo tangu Machi 17 baada ya masuala ya michezo kusimamishwa na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kurejea kuanzia Juni Mosi.Bodi ya Ligi iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) imesema kuwa Juni 13 masuala ya ligi yataaza rasmi.
Dilunga ni miongoni mwa wazawa wenye kazi ya kuanzia pale ambapo waliishia wakati ligi ikisimama.
Wakati Simba ikiwa imetupia mabao 63 amehusika kwenye mabao 9 akifunga mabao sita na kutoa pasi tatu za mabao.
Katika mabao hayo sita bao lake la kwanza msimu huu aliwatungua Lipuli wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Uwanja wa Uhuru kwa mkwaju wa penalti.
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandernbroeck amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na anaamini kuwa watarejea kwenye ubora wao baada ya muda mfupi
Post a Comment