CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba yupo kwenye mchakato wa kurejea nchini ili kuungana na wachezaji wenzake ambao wameingia kambini leo maeneo ya Mbweni.

Habari zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Simba umeanza mawasiliano na uongozi wa Serikali ya Zambia ili kujua namna ya kuweza kumpata nyota huyo kupitia Wizara ya Habari ya nchini Zambia.

"Tayari uongozi wa Simba umeanza mawasiliano na uongozi wa Serikali ya Zambia kupitia Wizara ya michezo ili kujua namna itakayofaa kumpata Chama, inawezekana na mambo yatakuwa sawa," ailieleza taarifa hiyo.

Jana, Meddie Kagere raia wa Rwanda aliwasili nchini na leo anatarajia kujiunga na wenzake ambao wapo kambini kuanza mazoezi.

Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa mpango wa kuwarejesha wachezaji upo na kila kitu kikiwa sawa mambo yatawekwa hadharani. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.