HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa hakuna shida kwao kucheza mechi zilizobaki jijini Dar es Salaam.
Masuala ya michezo yalisimamishwa tangu Machi 17 ambapo hakukuwa na mechi yoyote ya ushindani iliyochezwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa anaamini kwamba kilichotokea kwa sasa ni dharula hivyo hakuna kilichoharibika.
"Ujue kwa sasa hakuna ambacho unaweza kulaumu kwani ni dharula na hakuna ambaye alipanga kwa kuwa imetokea basi sisi tutapambana kupata matokeo mazuri kwani mpira ni dakika tisini," amesema.
Ligi tatu zimeruhusiwa kuanza ambazo ni Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo zitachezwa kwa mtindo wa vituo, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho zitachezwa Dar na Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zitachezwa Mwanza
Post a Comment