RAZACK Abarola, mlinda mlango namba moja wa Azam FC mikono yake ya dhahabu imepotezwa na mlinda mlango wa Simba Aishi Manula kwa upande wa kukusanya clean sheet pamoja na dakika za kukaa ndani ya uwanja.
Azam FC ikiwa imecheza mechi 28 ambazo ni dakika 2,520 amekaa langoni kwenye mechi 15 ambazo ni dakika 1,350 akikosekana kwenye mechi 13 huku Manula kwenye mechi 28 akikaa langoni mechi 21 ambazo ni dakika 1,890 akikosekana kwenye mechi saba.
Kwa upande wa Clean sheet Manula ametoka na jumla ya 13 huku Abarola akiwa nazo 8. Pia kipigo kikubwa cha Manula ni mabao mawili, ilikuwa sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Yanga, Januari 4 huku Abarola akipokea kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Simba.
Hizi hapa clean sheet 13 za Manula ilikuwa ni mbele ya Kagera Sugar 0-3 Simba, Biashara United 0-2 Simba,Simba 1-0 Azam FC, Singida United 0-1 Simba, Simba 4-0 Mbeya City, Simba 0-0 Prisons, Ruvu Shooting 0-3 Simba, KMC 0-2 Simba, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Lipuli 0-1 Simba, Simba 1-0 Kagera Sugar, Simba 2-0 KMC, na Simba 8-0 Singida United.
Hizi hapa clean sheet 8 za Abarola:-Azam 1-0 KMC, Polisi Tanzania 0-1 Azam FC, Yanga 0-1 Azam FC, Kagera Sugar 0-0 Azam FC, Mwadui 0-1 Azam FC, Azam 2-0 Lipuli, JKT 0-1 Azam FC, Azam FC 1-0 Polisi Tanzania
Post a Comment