UONGOZI wa Klabu ya Lipuli yenye ngome yake mkoani Iringa umesema kuwa utapambana kufikia malengo yake kwenye mashindano yote ili kumaliza ligi ikiwa ndani ya 10 bora.
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ndani ya Klabu ya Lipuli, Wille Chikweo amesema kuwa kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa Machi 17 kutokana na Janga la Virusi vya Corona hawakuwa na mwendo mzuri jambo ambalo wamelifanyia kazi.
Chikweo amesema kuwa baada ya Serikali kuruhusu ligi kuendelea Kamati ya Mashindano imeanza kuandaa mpango kazi utakaowapa matokeo chanya kwenye mechi zilizobaki jambo wanaloamini litawafanya wamalize ligi wakiwa nafasi nzuri.
Lipuli iliyo chini ya Kocha Mkuu Nzeyimana Mailo imeshinda mechi tisa na sare sita ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi 29 na kibindoni ina pointi 33 kinara wao wa utupiaji ni Paul Nonga mwenye mabao 11
Post a Comment