KLABU ya Simba ambao ni mabingwa watetezi, Mei 27 wanatarajia kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kutetea taji lao la ligi pamoja na kulisaka Kombe la Shirikisho.
Mazoezi hayo watayafanyia Mo Simba Arena yenye viwanja viwili vya nyasi za bandia na asilia.
Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni Mosi.
Mechi zote za ligi zitachezwa Dar ambapo viwanja vitatu vitatumika ule wa Uhuru, Azam Complex na Taifa
Post a Comment