SALUM Kimenya, beki kiraka wa Klabu ya Tanzania Prisons amesema kuwa kinachokwamisha dili lake la kutua ndani ya Simba ni dau kuwa chini kuliko lile analohitaji.
Kimenya amekuwa kwenye sarakasi za kujiunga na Simba mara nyingi ila mwisho wa siku anabaki kuendelea kukipiga ndani ya Prisons.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya ambaye anaurafiki mkubwa na nyavu kwa mabeki alisema kuwa dau limekuwa likikwamisha dili lake kuibukia Simba.
“Nimekuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya timu ikiwa ni pamoja na Simba ila kilichoshindikana ni upande wa maslahi tu ndio maana unaniona bado nipo hapa nilipo wakati wa kuondoka ukifika nitatoka tu,” amesema Kimenya.
Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake 41 na mabao 26 yeye amefunga mabao manne.
Post a Comment