BARAKA Majogoro nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania amesema kuwa sababu kubwa ya kuchagua kutumia jezi namba 15 uwanjani ni kuikumbuka siku yake aliyoletwa duniani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Majogoro amesema kuwa anapenda kuitumia jezi hiyo kwa kuwa anakumbuka tarehe aliyoletwa duniani.

"Napenda kuitumia jezi namba 15 kwa kuwa ni namba ya tarehe ambayo nililetwa duniani hivyo nikiwa nayo mgongoni ninapenda na ninakumbuka siku yangu ya kuletwa duniani.

"Nililetwa duniani Mei 15 hivyo ninaienzi siku kwa kuiweka mgongoni na kufanya kile ambacho ninakipenda siku zote," amesema.

Kiungo huyo amekuwa kwenye ubora wake na tayari ameshaanza mazoezi na timu ya Polisi Tanzania baada ya Serikali kuruhusu shughuli za michezo kuanza.

Hakukuwa na mechi ya ushindani tangu Machi 17 baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivuruga dunia. 

Tayari masuala ya michezo yaeruhusiwa kuanza ifikapo Juni Mosi na Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Juni 13

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.