Bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho ambaye ni Azam FC atakutana na Simba.
Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime itamenyana na Yanga iliyo chini ya Luc Eymael.
Alliance itamenyana na Namungo huku Sahare All Stars ambayo ni timu pekee inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kutinga hatua ya robo fainali itamenyana na Ndanda.
Hivi ndivyo Yanga na Simba zitakavyoweza kukutana:-
Mshindi wa mechi kati ya Simba na Azam atakutana na mshindi kati ya mechi ya Yanga na Kagera Sugar, hivyo ili hawa watani wajadi wakutane ni lazima kila mmoja ashinde mechi yake ili wakutane hatua ya nusu fainali.
Kwa upande wa Alliance na Namungo wao mshindi nusu fainali atamenyana na yule atakayeshinda mechi kati ya Ndanda na Sahare All Stars.
Post a Comment