MBARAKA Yusuph, mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa yupo vizuri kuendelea kupambana kwenye mechi za ushindani.
Mbaraka alikuwa nje akitibu majeraha yake aliyopata wakati akiwa ndani ya Klabu ya Namungo kwa mkopo msimu uliopita kwa sasa ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mbaraka amesema kuwa wakati wa mapumziko ya ligi yaliyotokana na janga la Virusi vya Corona alikuwa anafanya mazoezi binafsi na sasa yupo kambini.
"Nilikuwa ninafanya mazoezi binafsi nilipokuwa nyumbani na sasa tayari ninaendelea vizuri nikiwa kambini na wachezaji wenzangu, kikubwa ni kuendelea kupambana na kumuomba Mungu ili tuzidi kuwa salama," amesema
Post a Comment