UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una imani ya kufanya maajabu pale Ligi Kuu Bara itakaporejea Juni Mosi kwa wachezaji wao kujituma kupata matokeo ili kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa kama ilivyo kwa wapinzani wao Simba ambao ni mabingwa watetezi.
Ligi kuu wakati inasimamishwa, Yanga ilikuwa na pointi 51 ikiwa imecheza mechi 27 ikiachwa kwa pointi 20 na vinara Simba ambao wamecheza mechi 28.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kurejea kwa ligi kunamaanisha kwamba ile burudani ambayo walianza kuitoa inarejea.
“Burudani inarejea tuliikosa kwa muda mrefu, tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zilizobaki hivyo tukichanga karata zetu tunaweza kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na lile la Kombe la Shirikisho.
“Kila kitu kinawezekana kikubwa ni mashabiki kutupa sapoti na kuendelea kuwa nasi bega kwa bega, wachezaji wetu wanaari kubwa na nguvu ukizingatia kwamba walikuwa wanaendelea na mazoezi,watakapowasili kambini mipango yote itapangwa,” amesema Nugaz.
Post a Comment