MTENDAJI Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, amepiga bonge la biti kwa timu zote ambazo wamebakisha nazo mechi katika Ligi Kuu Bara kwa kuziambia kwamba hawataruhusu kuachia pointi yoyote ile.
Senzo amejigamba kwamba wanataka kumaliza ligi kibabe kwa kushinda katika mechi zao 10 ambazo wamezibakisha kabla ya msimu huu wa ligi kumalizika.
Senzo, raia wa Afrika Kusini,amesema kuwa wanataka kumaliza mechi hizo kibabe kwa kuhakikisha kwamba hawapotezi pointi yoyote na wana uhakika wa kufanya hilo kutokana na ratiba ya programu ambazo wachezaji wao walikuwa wanazifanya wakati ambao walikuwa nyumbani.
“Kitu kimoja tunachotaka kufanya ni kuwa tunahitaji kushinda kila mechi ambayo iko mbele yetu katika wakati huu ambao ligi inarejea.
“Tuna uhakika wa kulifanya hilo kwa sababu tulikuwa na programu nzuri wakati ambao ligi ilisimama na wachezaji walikuwa wanazifuatisha, kwa hiyo hatuna shida ya kuona kwamba tutashinda mechi zetu hizo zilizobakia,” alisema.
Post a Comment