SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anahitaji siku 21 ambazo ni sawa na saa 504 kwa ajili ya kukiaandaa kikosi chake kurejea kumalizia mechi 10 za Ligi Kuu Bara zilizobaki.
Masuala ya michezo ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza, la Pili, Ligi ya Wanawake, Ligi ya Mikoa yalisimamishwa na Serikali Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ila kwa sasa Serikali imeruhusu shughuli hizo kuanza ifikapo Juni Mosi.
Juzi, wachezaji wa Simba waliwasili kambini rasmi na kufanyiwa vipimo vya afya kisha walifanya mazoezi katika uwanja wao uliopo Bunju ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya mechi za Kombe la Shirikisho pamoja na ligi.
Sven amesema:- “Wachezaji wanahitaji wapate muda wa wiki tatu ili kujiweka sawa miili yao na mazoezi ukizingatia kwamba wamekaa muda mrefu bila mechi za ushindani hivyo ili miili yao irejee kwenye ubora ni lazima wapate muda wa kuirejesha kwa wakati.
“Nina amini ikiwa itakuwa hivyo basi kila kitu kitakwenda sawa na miili ya wachezaji itakuwa tayari kuanza kupambana kwenye mechi ngumu, malengo yetu ni kuona tunafanya vizuri kwenye mechi zetu zote tupo tayari.”
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 71 na imefunga jumla ya mabao 63 na kinara wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao 19.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.