SALUM Abubakari,’Sureboy’ kiungo anayetajwa kuingia kwenye rada za Yanga anayekipiga ndani ya Klabu ya Azam FC amemkalisha jumlajumla nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi kwenye mchango wake wa mabao ndani ya timu.
Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ikiwa imecheza mechi 28 imetupia kimiani jumla ya mabao 37 huku Sure Boy akihusika kwenye mabao matatu kwa upande wa Tshishimbi, Yanga ikiwa imefunga mabao 31 baada ya kucheza mechi 27 amehusika kwenye bao moja.
Sure Boy alimtengenezea pasi mbili, Obrey Chirwa kwenye mchezo dhidi ya KMC wakati wakishinda kwa mabao 3-1 na alitengeneza pasi moja aliyompa Joseph Mahundi wakati Azam FC ikishinda mabao 2-0 mbele ya Lipuli.Tshishimbi ana pasi moja ya bao aliyompa Tariq Seif kwenye mchezo wa Biashara United wakati wakishinda kwa bao 1-0.
Kwa upande wa mechi alizocheza kati ya 28 ni 23 na alikosekana kwenye mechi tano huku Tshishimbi naye akicheza mechi 23 akikosekana kwenye mechi nne.
Hizi hapa mechi za Sure Boy:-KMC, Polisi Tanzania, Ndanda, Namungo, JKT Tanzania, Simba,Yanga, Biashara United, Kagera Sugar, Ruvu Shooting, Alliance, Mwadui, Mtibwa Sugar, Lipuli, Mbeya City, Prisons, KMC, Coastal Union, Ndanda, Namungo, JKT Tanzania, Simba,  Ruvu Shooting.
Hizi hapa mechi za Tshishimbi:-Ruvu Shooting, Mbao FC , JKT Tanzania, Mbeya City, KMC , Prisons, Biashara United , Ndanda, Alliance, Simba , Azam FC, Singida United, Mtibwa Sugar, Lipuli, Ruvu Shooting, Mbeya City, Prisons , Polisi Tanzania, Coastal Union ,Mbao, Simba, KMC, Namungo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.