SVEN Vandernbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa amemrudisha nyumbani kiungo mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu kutokana na kosa la kuchelewa kambini.
Wachezaji wa Simba waliripoti kambini Mei 27 ambapo walipofika walifanyiwa vipimo na kuanza mazoezi jioni kwa kufanya mazoezi mepesi.
Sven amesema kuwa Ajibu hakutoa taarifa jambo lililosababisha amsimamishe kwa muda atamrejesha kikosini pale atakapoona inafaa.
Ajibu ndani ya Simba amefunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao aliibukia kikosini hapo akitokea Yanga msimu wa 2019/20
Post a Comment