NICOLAS Wadada beki wa Azam FC ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni ambao kwa msimu huu wa 2019/20 wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo.
Beki huyu wa kulia raia wa Uganda ni miongoni mwachezaji makini ndani ya uwanja.
 Azam FC ikiwa imefunga mabao 37 amehusika kwenye mabao nane ambapo ametoa pasi saba na kufunga bao moja.
Uwezo wake mkubwa wa beki huyo mwenye rasta ni kutumia guu lake la kulia pamoja na kushoto ambapo aliwatungua Biashara United wakati Azam FC ikishinda kwa mabao 2-1 Uwanja wa Chamazi.
Kwa sasa yupo zake nchini Uganda ambapo aliibuka huko baada ya janga la Virusi vya Corona anatarajiwa kurejea nchini pale mipaka itakapofunguliwa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.