MSHAMBULIAJI wa Inter Milan, Mauro Icard anayekipiga kwa mkopo ndani ya Paris Saint-Germain (PSG) inaelezwa kuwa anataka kubaki jumla ndani ya timu hiyo.

Raia huyo wa Argentina, alijiunga na mabingwa wa Ligue 1 mwanzoni mwa msimu wa 2019-20 akitokea Inter Milan amecheza jumla mechi 31 na kutupia mabao 20.

Bosi wa PSG Thomas Tuchel, inaelezwa kuwa ameanza mpango wa kufanya naye mazungumzo ili abaki ndani ya kikosi hicho.

Mshambuliaji huyo amekuwa ni mbadala wa Edinson Cavan wakati alipokuwa na majeraha kabla ya masuala ya michezo kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.


Amekuwa na muunganiko mzuri ndani ya kikosi wakiunga utatu wao dhidi ya Kylian Mbappe na Neymar ambao wote ni washambuliaji

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.