UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wapo kamili kwa ajili ya kuendelea na ligi pamoja na Kombe la Shirikisho baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo kuanza Juni Mosi.

Machi 17 Serikali ilisimamisha masuala ya mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.

Ofisa Habari wa Yaga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ayari wachezaji wameanza kuwasili kambini na watafanyiwa vipimo pamoja na semina kuhusu namna ya kujilinda na Virusi vua Corona.

"Tupo tayari na tuna zoezi endelevu la kuwapokea wachezaji wetu pamoja na kuwafanyia vipimo, walianza kuwasili jana na leo pia wataendelea kufanyiwa vipimo pamoja na kupewa elimu namna ya kujilinda na Corona.

"Kikubwa ni kwamba kila mmoja yupo tayari kuona kwamba anapambana kwa ajili ya timu kufanya vizuri pamoja na afya yake kuwa salama hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kipo sawa," amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 27 kibindoni ina pointi 51.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.