YOHANA Mkomola, nyota Mtanzania anayekipiga ndani ya FK Vorkslka Poltava timu ya chini ya miaka 21amesema kuwa janga la Virusi vya Corona limetibua mipango yake ya kutua Bongo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mkomola amesema kuwa alikuwa na hesabu za kurejea Tanzania ila kutokana na Corona mipango imevurugika.

"Nilikuwa na mpango wa kurudi Bongo ila kwa sasa inabidi nisubiri mambo yakae sawa kwani hakuna kutoka nje kutokana na mipaka kufungwa ila imani yangu ni kwamba mambo yatakuwa shwari.

Mkomola ametumia dakika 638 baada ya kucheza mechi 14.
Ametupia mabao sita na kutoa pasi mbili za mabao ana wastani wa kucheka na nyavu kila baada ya dakika 106

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.