LIGI Kuu England inatarajiwa kurejea rasmi Juni 17 kwa mechi mbili ambazo zilikuwa viporo kati ya Manchester City dhidi ya Arsenal na ule kati ya Aston Villa dhidi ya Sheffield.
Mechi nyingine zitaendelea kurindima Juni 20 huku mpango wa kumalizia ligi hiyo ambayo mabingwa watetezi ni Klabu ya Manchester City ikitarajiwa kumalizika mapema mwezi Agosti.
Aston Villa ambayo anakipiga nahodha wa timu ya Tanzania, Mbwana Samatta ina kibarua kizito cha kupambana ili kubaki ndani ya ligi msimu ujao kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri.
Ikiwa imecheza mechi 28 imejikusanyia jumla ya pointi 25 kibindoni itapambana na Sheffield iliyo nafasi ya saba kwenye msimamo na kibindoni ina pointi 43.
Hakukuwa na mchezo wa kiushindani tangu Machi 13 kutokana na janga la Corona ambalo linaivurugavuruga dunia na mechi zao zitakuwa bila mashabiki ili kuendelea kuchukua tahadhari.
Post a Comment