MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismael Aden Rage anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo ilisema kuwa mnamo Mei 23, 2020, Rage ambaye ni Mkurugenzi wa Voice of Tabora alishikiliwa baada ya TAKUKURU kupata taarifa kutoka chanzo cha siri kikieleza kuwa Mbunge huyo wa zamani wa Tabora Mjini amedaiwa kuanza kampeni za uchaguzi kabla ya wakati.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya siri iliyotolewa ilieleza kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Simba akiwa katika maeneo kadhaa ndani ya manispaa ya Tabora kwa nyakati tofauti alikusanya wapiga kura ambao ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazoi ya kata na matawi kwa lengo la kuwashawishi ili wampigie kura.
“Ili kutoharibu uchunguzi unaondelea, Rage aliwekwa mahabusu kuanzia juzi Mei 23 hadi jana Mei 24 ambapo aliachiwa kwa dhamana.
“Uchunguzi wa taarifa hii unaendelea na mara utakapokamilika taarifa kamili itatolewa kupitia vyombo vya habari,” ilieleza taarifa hiyo ya Mkuu wa Takukuru mkoa Tabora, Mussa Chaulo.
Hata hivyo taasisi hiyo imewataka wanaokusudia kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi ,kuu wa Oktoba 2020 waache mara moja kutoa rushwa na kufanya kampeni kabla ya wakati na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na sheria namba 11 ya mwaka 2007.
Chaulo alisema, “Niwatake wananchi wasikubali kurubuniwa na wanaokususdia kugombea nafasi mbalimbal za uongozi, tumebaini kuwa kuna watu wameanza kujipiitisha kwa lengo la kuwarubuni wananchi na kuwahonga ili wawapigie kura wakatiu wa kura za maoni.”
Post a Comment