IKIWA imebaki takribani wiki moja kufi kia Juni Mosi, mwaka huu siku ambayo ligi za hapa nchini zitarejea, Serikali, Bodi ya Ligi (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana Jumamosi walikutana na kujadili namna gani wataweza kudhibiti Virusi vya Corona pindi michezo hiyo itakapoanza.

 

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo alikuwepo kwenye kikao hicho maalumu kwa ajili ya kuona namna gani wataweza kupambana na Virusi vya Corona viwanjani na kutaka kujua Wizara ya Afya wamejipangaje na jambo hilo kabla ya kuanza kwa ligi zenyewe.

 

Kikao hicho ambacho kilizikutanisha Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Afya pamoja na viongozi wa TFF na wa Bodi ya Ligi, kilifanyika katika Ofi si za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizopo Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Singo alisema, hakikuwa kikao cha kutoa ratiba ya ligi, bali walitaka kujua ni vitu gani ambavyo vitahitajika kwa wanamichezo na mashabiki katika wakati huu wa kupambana na Virusi vya Corona, licha ya kuwa TFF na TPLB walikaribishwa kusikiliza mchakato huo ili na wao wajue wanaisaidia vipi Serikali wakati michezo hiyo itakapoanza.

 

“Kikao chetu hakikuwa cha kupanga ratiba kwa sababu wanaohusika na hizo ratiba na muundo wa ligi ni TFF na TPLB na mamlaka za soka zinazohusika, sisi kikao chetu ilikuwa ni kujadili misingi ya kiafya itakuwaje pindi ligi itakapoanza.

 

“Yaani tunajadili ni mfumo gani ambao utakuwa sahihi kuutumia ambao utakuwa unazilinda klabu, wachezaji na mashabiki wakati wa ligi, kwa hiyo TFF na BMT wao tumekaribisha kuja kusikiliza kile ambacho sisi tunakijadili, mambo ya ratiba na ligi itakuwaje hiyo ipo juu ya TFF na Bodi ya ligi wenyewe,” alisema Singo.

 

Spoti Xtra lilimtafuta Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Stephen Mguto, kutaka kujua ratiba ipoje, lakini alisema hayupo kwenye kikao atafutwe, Ofi sa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo.

 

Alipotafutwa Kasongo, simu yake iliita bila ya kupokelewa ingawa taarifa zinasema kuwa, ishu ya ratiba na mambo yote kuhusu ligi, yatafahamika kesho Jumatatu.Ikumbukwe kuwa, baada ya kutangazwa michezo kuendelea Juni Mosi, mwaka huu, imepangwa Ligi Kuu Bara kuchezwa Uwanja wa Taifa, Uhuru na Azam Complex jijini Dar, huku Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuchezwa Nyamagana na CCM Kirumba jijini Mwanza

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.