MAISHA yanakwenda kasi sana kwa sasa ila mambo mengi yanaonekana kusimama kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaitikisa dunia kwa sasa.
Kwa Bongo Machi 17, ligi mbalimbali zilisimamishwa na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ikiwa ni hatua za kudhibiti maambukizi zaidi ya Corona.
Wakati ligi inasimamishwa kuna wachezaji ambao walikuwa kwenye ubora wao na walikuwa wakifanya vizuri, tayari burudani inatarajiwa kuanza tena Juni Mosi, hiki hapa kikosi matata kabala ya Corona:-
Aishi Manula wa Simba
Timu ya Simba ikiwa imecheza mechi 28, Manula amekaa langoni kwenye mechi 21. Simba ikiwa imefungwa mabao 15 amefungwa mabao 10.
Ana clean sheet 13  mbele ya:- Kagera Sugar 0-3 Simba, Biashara United 0-2 Simba, Simba 1-0 Azam FC, Singida United 0-1 Simba, Simba 4-0 Mbeya City, Simba 0-0 Prisons, Ruvu Shooting 0-3 Simba, KMC 0-2 Simba, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Lipuli 0-1 Simba, Simba 1-0 Kagera Sugar, Simba 2-0 KMC, Simba 8-0 Singida United.
Ametunguliwa mechi nane mbele ya :-Simba 3-1 JKT Tanzan ia, Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Mwadui 1-0 Simba, Simba 0-1 JKT Tanzania, Simba 2-2 Yanga, Biashara United 1-3 Simba, Azam FC 2-3 Simba, Yanga 1-0 Simba.
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba
Beki wa kushoto wa Simba, amecheza mechi 18 ambazo ni dakika 1,620 amehusika kwenye mabao manne yalifungwa na Simba kati ya 63 ambapo amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao licha ya kuwa ni beki.
Kelvin Yondani wa Yanga
Uzoefu unambeba kwani ni mchezaji ambaye amedumu muda mrefu ndani ya Yanga akiwa katika ubora wake na amekuwa mfano kwa mabeki wengi ndani ya uwanja.Kiongozi mzuri kwa wenzake na anauwezo wa kutuliza timu pale inapokosa utulivu.
Bakari Mwanyeto wa Coastal Union
Chipukizi ambaye anaaminiwa na Kocha Mkuu wa Coastal Union akiwa ni kiongozi wa ulinzi ndani ya klabu yake. Safu yake ya ulinzi imefungwa mabao 19 baada ya kucheza mechi 28. Licha ya kuwa ni beki ametupia bao moja kati ya mabao 27 yaliyofungwa na Coastal Union.
Nicolas Wadada wa Azam FC
Beki huyu wa kulia raia wa Uganda ni miongoni mwachezaji makini ndani ya uwanja. Azam FC ikiwa imefunga mabao 37 amehusika kwenye mabao nane ambapo ametoa pasi saba na kufunga bao moja.
Haruna Niyonzima wa Yanga
Licha ya kuwa ni ingizo jipya ndani ya Yanga kwani alitua kwenye dirisha dogo anaitambua vema ligi ya Bongo na mechi za kimataifa ana uzeefu nazo. Amecheza mechi 14 na ametupia bao moja ndani ya Ligi Kuu Bara huku akitumia dakika 1,247 uwanjani.
Mechi zake hizi hapa:-Simba (90), Kagera Sugar (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mtibwa Sugar (90), Lipuli (84), Ruvu Shooting (90), Mbeya City (90), Prisons (90), Polisi Tanzania (85), Coastal Union (88) Alliance (90), Simba (90), KMC (90)
Papy Tshishimbi
Kiungo huyu ni jembe la kazi kwani amekuwa ni bora muda wote ndani ya uwanja, kwenye ligi amecheza mechi 23 wakati Yanga ikiwa imecheza mechi 27. Ametumia dakika 1,936 na ana pasi moja ya bao.
Mechi zake hizi hapa:-Ruvu Shooting (90), Mbao FC (90), JKT Tanzania (90), Mbeya City (90), KMC (90), Prisons (26), Biashara United (20), Ndanda (90), Alliance (90), Simba (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mtibwa Sugar (90), Lipuli (90), Ruvu Shooting (90), Mbeya City (90), Prisons (90), Polisi Tanzania (90). Coastal Union (90) ,Mbao (90), Simba (90), KMC (90), Namungo (90)
Jonas Mkude wa Simba
Kiungo mzawa ambaye ana uwezo mkubwa ndani ya uwanja. Amecheza jumla ya mechi 16 sawa na dakika 1,440 kati ya 28 ambazo Simba imecheza.
Amehusika kwenye mabao manne ya Simba akifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao kati ya 63 yaliyofungwa na Simba.
Bernard Morrison wa Yanga
Ingizo jipya ambalo limeweza kufanya maajabu ghafla kwa muda mfupi ndani ya ligi akiwa amecheza mechi 10 na kutumia dakika 852. Amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.
Mechi zake hizi hapa:-Singida United (90), Mtibwa Sugar (85), Lipuli (90), Ruvu (81), Prisons (90), Polisi Tanzania (90), Mbeya City (90) na Alliance (90), Simba (56), Namungo (90).
Kagere
Meddie Kagere wa Simba Mtambo wa mabao ndani ya Simba akiwa ni kinara wa kutupia msimu huu kibindoni ana mabao 19 na pasi tano za mabao akiwa ametumia dakika 2,131. Simba ikiwa imecheza mechi 28 amekosekana kwenye mechi mbili pekee.
Mechi zake:-JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (87), Biashara United (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mwadui FC (90), Mbeya City (90), Prisons (90), KMC (90), Ruvu Shooting (75), Lipuli (90), Yanga (68), Mbao (90), Alliance (90), Namungo (90), Coastal Union (90), Polisi Tanzania (14), JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), Lipuli (79) Azam (29), Yanga (69) na Singida (90)
Paul Nonga wa Lipuli
Mzawa huyuanayekipiga Lipuli anaingia kwenye orodha ya kikosi bora kabla ya janga la Virusi vya Corona kwa kuwa alikuwa anakuja kwa kasi na uwezo wa kucheka na nyavu pamoja na kutengeneza pia.
Ametupia jumla ya mabao 11 huku akiwa na pasi nne za mabao ndani ya Lipuli.
Akiba
Razack Abarola wa Azam FC
Salum Kimenya wa Tanzania Prisons
Bruce Kangwa wa Azam FC
Juma Abdul wa Yanga
Lukas Kikoti wa Namungo
John Bocco wa Simba

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.